ELEWA KUHUSU BITCOIN & CRYPTOCURRENCIES.
Pata mwanga juu ya hii biashara.
Kama wewe ni mgeni kwenye biashara hii ya digital currency soma makala hii mpaka mwisho!! Nitaanza na kueleza mapito ambayo mwanadamu amekuwa akipitia kwenye kubadilishana bidhaa yoyote na fedha au vito!!1.Barter trade system. Wengi tunajua mfumo huu wa manunuzi na mauzo ya vitu uliojulikana kama Barter Trade. Barter trade ni mfumo ambao watu walibadilishana bidhaa kwa bidhaa, hapakuwa na fedha kama sasa. Kwa hiyo ukihitaji nguo inabidi umpe anayeuza nguo kile ulichonacho mfano mnabadilshana nguo kwa kuku, mahindi kwa mbuzi na kadhalika. Mfumo huo ukapita ukaja mfumo mwingine!!
2.Vito vyaThamani kama Dhahabu. Ulimwengu ulihama kutoka kwenye zama za kubadilisha vitu kwa vitu ukahamia kwenye kubadilisha vitu kwa KITO cha thamani kama dhahabu. Thamani ya vipande vya dhahabu ilipimwa kwa wingi au ubora wa bidhaa husika inayobadilishana na kipande hicho cha dhahabu. Mfumo huu au zama hizo zikapita. Ukaja mfumo mwingine!! Endelea kusoma.....
3. Coin and Paper money Age. Matumizi ya dhahabu bado yalikuwa magumu sana. Wizi na ugumu wa kusafiri na vipande vya dhahabu viliifanya dunia kuja na mfumo wa sarafu na fedha za makaratasi. Mfumo huu ndo ambao tunautumia kwa kiasi kikubwa mpaka sasa. Mfumo huu umedumu sana kwa karne nyingi!! Hata hivyo, mfumo huu unaendelea kukosa nguvu. Tangu miaka ya 2005 mfumo mpya wa kutembea na Phone Wallets au mobile money umedhoofisha sana mfumo wa paper note au coin money!!
4. Mobile Money Age. Huu ni mfumo ulioletwa na Internet na Mobile phones. Mfumo huu umeanza miongo kama miwili iliyopita yaani mwisho mwa miaka ya 1990. Mfano wa Mobile Money ni: Western Union, MPESA, Tigo Pesa, Airtel Money, Simbanking, Pesa Fasta, na mifumo mingine mingi ya kutuma, kupokea, na kutumia pesa kwa kutumia mitandao ya simu na internet au simu. Mobile Money imeleta mageuzi makubwa sana kwenye mfumo wa fedha duniani. Fedha inahamishika kirahisi. Biashara nyingi zimekuwa rahisi kwa sababu ya matumizi ya Mobile Money au Mobile Banking. Mfumo huu nao unataka kufika kwenye kilele chake!! Mfumo ufuatao ndio unaenda kutawala tena ulimwengu wa biashara na sekta ya fedha! Hebu twende pamoja!!!!!
5. CryptoCurrency Age.
Ngoja nitoe mfano wa mobile money inavyoweza kutumika kama digital money. Umewahi kwenda sehemu ukaona wameandika lipa hapa kwa Tigopesa? Yaani kama una hela kwenye Tigopesa au Mpesa unalipia huduma au bidhaa bila kutoa sarafu au noti (actual coins or paper note)?
Unaweza Kupata chakula hotelini na ukalipia huduma hiyo bila kutoa noti mfukoni mwako!! Nk.
Umewahi kuona kwenye super markets watu wananunua bidhaa au huduma kwa kutumia master au visa cards bila kutoa fedha mfukoni? Hivyo ndivyo Cryptocurrency itakavyofanya kazi siku zinazokuja kuanzia sasa!! Swali, kama Mobile Money ipo, Cryptocurreny ya nini tena? Jibu ni kwamba, Cryptocurrency ina faida nyingi naomba nitaje baadhi tu:
1. Kutuma na kupokea fedha ni sawa na bure kabisa duniani kote kwani ada/fee ya kutuma ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya mabenki!!!
2. Kutuma na kupokea pesa ni kwa haraka kama unavyotuma na kupokea ujumbe wa email kwenye internet au WhatsApp na Twitter!
3. Cryptocurrency inatumika dunia nzima wakati mobile money nyingi zinatumika eneo husika tu ambapo mtandao wa simu upo. Mf MPESA
4. Mfumo wa Cryptocurrency ni madhubuti sana kwa hiyo ni ngumu sana kuibiwa (money laundering).
5. Akaunti yako ipo mikononi mwako, huna haja ya kwenda bank kuchukua fedha!! Je, katika mfumo huu mpya wa Sarafu duniani kuna fursa yoyote ndani yake? Jibu lake ni ndiyo, Kuna kampuni nyingi sana zipo kwenye sekta hii ya Crypto Currency zikifanya yafuatayo:
1. Exchanging digital currency with non digital currency!! Hii ni fursa kubwa sana. Changamkia
2. Trading Crypto Currency to Crypto Currency
3. Mining Crypto Currency using special software. Kinachofanyika hapo kampuni nyingi zimewekeza kwenye technology ya kuchimbua Sarafu za kidigitali kama Bitcoins, Ethereum, nk: Ukiwekeza kwenye kampuni hizo kadri Sarafu zinavyopatikana utapata Sarafu zako kulingana na mtaji wako uliowapatia kwenye kampuni!!
4. Become Agents for Crypto Currency to non Crypto Currency!! Hii ni fursa ya uwakala wa Sarafu ya Digitali kwa Sarafu za kawaida mfano Dollars, pounds, euro nk. Faida yake ni kubwa!! BY LEON ©2017 (0743854455)
UPEKEE WA BITCOIN (BTC) PAMOJA NA FAIDA ZAKE.
Bitcoin ni sarafu ya kidijiti inayowezesha malipo madhubuti na ya papo, kwa mtu yeyote, popote duniani. Ununuzi na kutoa bitcoin zinafanywa pamoja na mtandao. Bitcoin iligunduliwa mwaka 2009 na Satoshi Nakamoto. Bitcoin zimetambuliwa kama sarafu na mashirika mengi na hutumiwa kulipia bidhaa na huduma kuanzia kwa kusafirisha pesa kutoka nchi moja hadi nyingine. Kwa sasa kuna sarafu za milion 16.2+ za bitcoin duniani. Kila moja na thamani ya takriban $35,000+.
Bei inabadilika siku hadi siku kutokana na uwekezaji wa Bitcoin. Jinsi ya kuhifadhi bitcoin:
Unaweza kuihifadhi BITCON au CRYPTOCOIN kwenye online wallets mfano blockchain (https://blockchain.info) , na unaweza kuitumia kama pesa nyingine kulipia huduma na kununua bidhaa hasa mtandaoni. Pia baadhi ya nchi zinapatikana ATM za Bitcoin ambazo unaweza kubadili bitcoins zako na kuwa cash. Jinsi ya kupata Bitcoin:
Kuna sehem nyingi za kununua Bitcoins, unaweza kununua kwa kutumia credit au debit card yako, lakini mara nyingi ukitumia credit au debit card inachukua siku nyingi mpaka uje kupata bitcoins zako, njia rahisi kama unataka kununua ingia localbitcoins.com utakuta wauzaji wengi, pia unaweza kununua kwa mtu anayeaminika kupitia malipo ya fedha kwa mitandao mfano (Mpesa/tigopesa/airtelmoney).
UPEKEE WA BITCOIN (BTC)
1. Isiyo na mamlaka kuu: Bitcoin ni programu huria na la wazi chanzo. Hakuna mtu aliye na miliki yake, mteja maarufu inaimarishwa na jamii ya watengenezaji na tena teja nzingine nzuri zinapatikana. Aidha, mtandao hutumia mtandao madaraka ya maelfu ya sava na kompyuta.
2. Bitcoin huokoa fedha: Kutumia mtandao wa Bitcoin ni bure, ila kwa ajili ya ada ya hiari unayoweza kutumia ili kuharakisha usindikaji ya ununuzi.
3. Unaweza kuwekeza na kuuza Bitcoin mda wowote na kupata kipato: Faida huja pale unaponunua kipindi zinauzwa kwa bei ndogo na kuziuza kwa bei kubwa kipind zinapopanda duniani. Ina manufaa gani kwa wafanya biashara? Malipo ya Bitcoin yanaweza kukubalika popote duniani bila hatari ya malipo kugeuzwa. Ada ya chini inamaanisha kuwa unaweza kupitisha akiba ya juu kwa wateja wako na kupata faida zaidi ukijilinganisha na wafanyabiashara wengine. Manunuzi yaliyothibitika, zinahifadhiwa na mtandao mkubwa.
WAWEZA HIFADHI BTC ZAKO KWENYE ONLINE WALLETS KAMA:www.localbitcoin.com, www.blockchain.com nk
Mimi nina Bitcoin zangu nitafanyaje ziwe fedha za Tsh??
Naomba leo nitoe somo hili. Litumike kuwafahamisha wengine. Wale wazoefu mnafahamu kabisa, Bitcoin, DOGECOIN, RIPPLE , ETHEREUM kuwa ni pesa halali kwa malipo kokote duniani.
Tukubaliane hapo kwanza. Akili zetu zifunguke, ukisikia vitu hivyo, ujue hizo ni pesa. Pesa hizi zinaitwa pesa za kidigitali. Hazishikiki. Hazidhibitiwi na Bank wala nchi yoyote duniani. Uanze kuzoea kuziita Digital Currencyau Crypto Currency. Meza hiyo kichwani, mpe na mwenzio ajue. Dunia hii inabadilika haraka sana. Kuna msemo, if you don't want to change, changes will change you. Hii ndiyo teknologia, itatubadili sisi bila kutaka.
Kama tumekubaliana sote kwamba hizo ni pesa sasa je nizitoeje kwenye hizo porch (wallet)? Kuna namna mbalimbali ya kuzitoa Cryto currency kwenye Wallet yako:
1. Bitcoin inaweza kutoka kwa ATM machine hasa nchini China, Ulaya, Marekani na kwa baadhi ya nchi za Africa. ATM kwa Tanzania bado hazipo basi na kama zipo zitakuwa zinatumiwa na baadhi ya wakala/mawakala wa BITCOIN.
2. Bitcoin unaweza kuziuza online ukapata cash. Hii njia ndiyo watu wengi wanaitumia na ndiyo inaifanya Bitcoin isishuke thamani. Ukienda www.locabitcoin.com au www.remitano.com huko utaweza kuuza au kununua Bitcoin zako kwa mawakala ambao ni trusted sana.
LEON ©2017-2021 (0743854455 )
NICE CONTENT
ReplyDeleteNice content
ReplyDelete